THE BENJAMIN WILLIAM MKAPA HIV/AIDS FOUNDATION

Habari kuhusu THRP

E-mail Print PDF

JE, UNAFAHAMU KUWA SERIKALI YA TANZANIA IMEONGEZA NAFASI ZA AJIRA KWA WATUMISHI WA SEKTA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII?

  1. Katika kuboresha utoaji huduma bora za afya nchini na Ustawi wa Jamii, Serikali ya Tanzania imeendelea kutoa kipaumbele kwa  kuongeza idadi za ajira, kwa watumishi wa afya na ustawi wa jamii nchini, ikitumia  mikakati mbalimbali.
  2. Ili kuziba pengo la asilimia 62%  la uhaba wa watumishi wa afya na ustawi wa jamii,  Serikali ilipanga kuongeza idadi ya watumishi kulingana na  bajeti iliyotengwa kila mwaka, pamoja na maombi ya vibali vya ajira yanayowasilishwa na Halmashauri mbalimbali nchini.
  3. Kuanzia Julai 2005 hadi Juni 2010, jumla ya vibali vitano (5) vya ajira ya watumishi wa afya na ustawi wa jamii wa kada na ngazi mbalimbali vimetolewa na Serikali, vyenye idadi ya watumishi 23,502 kwa ngazi ya Taifa, Kanda, Mikoa na Halmashauri.Katika vibali hivyo, takriban asilimia 70 ya nafasi zilizotengwa, zilijazwa na watumishi ambao walipangiwa  kazi kwenye  vituo vya kazi mbalimbali nchini (Takwimu kutoka WAUJ, 2010).


             Takwimu, WAUJ,2010

       

MAENEO YANAYOHITAJI UIMARISHAJI

Pamoja na jitihada hizi za Serikali na wadau wengine, yapo  maeneo muhimu yanayohitaji kuimarishwa:

  1. Serikali na wadau wa Sekta ya Afya na Ustawi wa Jamii  waongeze vyuo zaidi na uwezo wa vyuo kudahili na kutoa wahitimu wengi zaidi, wenye taaluma mbalimbali za  afya pamoja na kubuni na kuimarisha mifumo ya kuwapangia kazi baada ya kuhitimu masomo, kuwafikisha kwenye vituo vyao vya kazi na kuwafanya wabakie huko.
  2. Halmashauri zitoe taarifa mapema, kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, kuhusu idadi na aina ya kada ya watumishi wapya, walioripoti kwenye vituo vya kazi.
  3. Halmashauri ziweke  takwimu sahihi ili kupata  mwelekeo wa watumishi wanaoripoti na kubaki katika vituo vyao
  4. Kuendelea kuelimisha Halmashauri zote juu ya  umuhimu wa kuwa wabunifu wa  kutengeneza mikakati ya kuvutia na kubakiza watumishi  wa afya na ustawi wa jamii kwenye vituo. Vivutio hivyo pia viwekwe  wazi  kwa jamii.
  5. Halmashauri kuhamasisha wadau wote wa sekta,  kuchangia katika ajira ya  watumishi kwa Mikataba kwa muda na hatimaye kuwaingiza katika ajira ya Serikali kama mpango wa muda mrefu, wa kuongeza idadi ya watumishi.

Ujumbe huu umetolewa na Taasisi ya Mkapa Foundation, kupitia Tanzania Human Resource Project, kwa msaada wa Watu wa Marekani,kupitia Shirika la Misaada la Marekani (USAID)
                                                                                                                      

Last Updated ( Wednesday, 02 February 2011 12:22 )  

In July 2005, then President of Tanzania, H.E. Benjamin William Mkapa and the former US President H.E. William Jefferson Clinton launched the Benjamin William National HIV/AIDS Fellows program. The aim was to recruit, train and deploy highly skilled health workers to server rural areas.

You are here: Home Programmes Tanzania HR Capacity THRP News in Kiswahili