TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

bmaf logo

TAASISI YA MKAPA FOUNDATION YAZINDUA RASMI AWAMU YA PILI YA MRADIWA MKAPA FELLOWS

Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/AIDS Foundation (BMAF) kwa ufadhili wa washirika wake mbalimbali yakiwemo mashirika ya maendeleo, makampuni na watu binafsi, imezindua rasmi awamu ya pili ya mradi wa Mkapa Fellows. Mradi huu unalenga kuimarisha huduma za ukimwi na afya ya mama na mtoto katika maeneo ya vijijini.

Itakumbukwa kuwa Taasisi ya BMAF ilifanya harambee mwezi Juni 2012 na kupokea ahadi za jumla ya Sh.3.2 bilioni ili kufanikisha hatua ya kwanza ya mradi. Kufuatia juhudi hizi, mradi huu umezinduliwa rasmi mwaka 2013.

Mradi wa Mkapa Fellows awamu ya 2 utatekelezwa kwa miaka mitano (2012-2017) na unalenga kuajiri “Fellows” ambao ni wataalam wa afya 150 na, makatibu wa afya 30 watakaofanya kazi kwenye wilaya 15 za Tanzania Bara na Zanzibar. Mradi pia unalenga kujenga na kuweka vifaa kwenye vyumba vya upasuaji 30 vitakavyotoa huduma za akina mama wajawazito. Aidha pia mradi huu unalenga kutoa mafunzo kwa Fellows na watumishi wengine waliopo kazini katika masuala ya ukimwi, kuzuia maambukizi ya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na Huduma ya dharura ya mama mjamzito.

Mradi wa Fellows utatekelezwa katika hatua mbili, ambapo hatua ya kwanza itakuwa kuanzia mwaka 2012 hadi 2014, na hatua ya pili itakuwa kuanzia mwaka 2015 hadi 2017. Katika hatua ya kwanza ambayo inaanza mwaka huu 2013. Jumla ya wataalam wa afya ( Fellows) 32 wataajiriwa na kwenda kufanya kazi katika vituo vya afya tisa (9) kwenye wilaya sita (6) za Sumbawanga Vijijini, Nkasi, Kalambo, Kahama, Kishapu na Biharamulo.

Kabla ya kwenda kwenye vituo vya kazi, Fellows hao watapatiwa mafunzo ya kutoa matibabu kwa wagonjwa wa ukimwi,na mafunzo hayo yatafanyika Iringa, mwezi Februari mwaka huu. Aidha mafunzo ya huduma ya dharura ikiwemo upasuaji kwa akina mama wajawazito, yatafanyika kwa miezi minne (4) kuanzia Juni 2013 , kwa Fellows watakaojiriwa na watumishi wengine waliopo kazini kwenye wilaya husika.

Hali kadhalika, ujenzi wa vyumba vya upasuaji nane (8) na ukarabati wa chumba kimoja (1) cha upasuaji vitaanza kuanzia mwezi Aprili 2013 katika Wilaya za mradi. Mradi huu pia utajumuisha utoaji wa huduma za mkoba, elimu ya afya na uhamasishaji kwa wanaume, wanawake na vijana wanaoishi kwenye maeneo ya jirani na vituo vya afya.

Taasisi ya BMAF inatoa shukrani za dhati kwa wadau mbalimbali waliochangia mradi huu. Shukrani za kipekee zinatolewa kwa “Irish Aid” kwa mchango wao mkubwa kwenye mradi huu. Pia tunashukuru makampuni mbalimbali ambayo yamechangia hatua hii ya kwanza ya mradi wa Mkapa Fellows zikiwemo; African Barrick Gold, Mfuko wa Pensheni wa NSSF, Bank M, Quality Group, Clouds Media, Benki ya NBC, NHIF na Benki ya Stanbic. Pia tunaishukuru, Precision Air, Pan African Energy Tanzania, Benki ya CRDB, Anglo Gold Ashanti , Shirika la PPF, Benki ya CBA Ltd na Benki Kuu ya Tanzania. Hali kadhalika tunatoa shukrani kwa Benki ya NMB, Kampuni ya Infotech Investment, Kampuni ya Manawa Ginneries , Benki ya TIB, Kampuni ya WIA Group, Grey Investment na Mfuko wa LAPF, SWISSPORT T Ltd, Bohari Kuu ya Madawa (MSD), Computer Connections, Kampuni ya Undi, Hoteli ya Nashera, Hoteli ya Kibo Palace na Karimjee Jivanjee Foundation.

Jitihada zaidi za harambee kwa ajili ya mradi huu zitaendelea mwaka huu wa 2013 ili kuweza kuziba pengo la Tsh 12.8 bn/=, zinazotarajiwa kuendeleza hatua ya pili ya mradi wa Mkapa Fellows. Tunawashukuru washirika wetu wote na tunatarajia kuendelea na ushirikiano, wakati tukianza mwaka huu 2013, na tunapozindua rasmi awamu ya pili ya mradi wa Mkapa Fellows katika wilaya 6 za mwanzo.

IMETOLEWA NA AFISA MTENDAJI MKUU TAASISI YA BENJAMIN WILLIAM MKAPA HIV/AIDS FOUNDATION.

MAELEZO KWA WAHARIRI:

Mkapa Fellows ni mradi bunifu ulioanzishwa hapa Tanzania na Watanzania na kutekelezwa na Taasisi ya Mkapa Foundation kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, wakiwemo Serikali ya Norway na Shirika la Clinton Foundation. Mradi huu umeweza kuvutia na kubakiza zaidi ya asilimia 90 ya watumishi wa afya walioajiriwa kufanya kazi kwenye wilaya 33 za Tanzania vijijini katika awamu ya kwanza ya mradi.

Katika awamu ya kwanza ya mradi ulioanza kuanzia mwaka 2005 hadi 2010, matokeo yalikuwa ongezeko mara tano ya idadi ya wagonjwa waliopatiwa huduma za madawa ya kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi katika wilaya ambazo Fellows walikuwepo kutoa huduma hiyo.. Zaidi ya Vituo 120 vya kutolea huduma kwa wagonjwa wa ukimwi viliongezeka kupitia uwepo wa Fellows. Asilimia 60 ya Fellows waliuhishwa katika ajira ya Serikalini na hivyo kuwepo na uendelevu wa jitihada zilizoanzishwa na mradi.

Serikali ya Tanzania ilitambua uwezo wa Taasisi ya BMAF katika kuchangia na uimarishaji wa masuala ya Raslimali watu katika sekta ya afya kwa kutumia miradi bunifu. Hali hii imepelekea ushirikiano zaidi kwenye miradi mingine, ukiwemo “Mradi wa ajira ya dharura”; na “Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Afya”ambayo yote miwili imefadhiliwa na Mfuko wa Dunia wa kupambana na ukimwi, kifua kikuu na Malaria ( Global Fund). Miradi hii miongoni mwa matokeo yake ni kuweza kuajiri zaidi ya watumishi 400 ambao wameimarisha huduma za Ukimwi, Kifua kikuu na Malaria nchini, kujenga nyumba za watumishi wa afya 90 katika vituo vya tiba nchini na mengi mengineyo.

Benjamin William Mkapa HIV/AIDS Foundation,

Masaki, Barabara ya Chole, Kitalu Na.372

S.L.P. 76274, Dar es Salaam,

Tanzania

Simu: +255 (22) 2600540/2/3, +255 (22) 2600531.

Barua Pepe: info@ mkapahivfoundation.org

www.mkapahivfoundation.org

 

Kwa Mawasiliano zaidi:

Ms. Sizarina Hamisi;

Simu: +255 22 2600590;

Barua Pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.


Donation

“Your contribution makes our work possible”

……………Donate now……………
Donate by phone or by e-mail, or to the account below:

Telephone: Tel:+255 22 2618557-9

Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

We will assist you with the process and answer any questions you may have about your contribution to our Foundation. Your contribution will enable smooth operation of the Mkapa HIV/AIDS Foundation activities at the sites to reach their clients easily.

We need your help today. Please send the most generous support you can afford to create a future of hope for the rural poor Tanzanians. The account to donate is shown below:

Account Name: Mkapa Fellows Program

Account Number: 0250008907

Bank Name: Bank M (Tanzania) Limited

Swift Code: BNKMTZTZ

Scroll Up